庚申講 International Project

Kiswahiliスワヒリ語版

Koshin-ko ni nini?

(庚申講) ni desturi ya jadi ya watu wa Japani.

Kwa mujibu wa Utao, dini iliyoanzia nchini China, mwilini mwa binadamu huishi wadudu watatu: mmoja kichwani, mmoja katika viungo vya ndani, na mmoja sehemu ya chini ya mwili. Wadudu hao watatu huitwa (三尸).

Inaaminika kuwa hao husababisha maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa na maradhi mengine. Si hayo tu: usiku wa (庚申), unaokuja mara moja kila baada ya siku 60, hutoka mwilini mwetu, hupanda mbinguni na kumpelekea mungu (天帝) taarifa ya matendo mabaya ya mwenyeji wao.

, anayeaminika kusimamia muda wa maisha ya binadamu, husikiliza taarifa za na kupunguza maisha ya mwenyeji kulingana na uzito wa makosa yake.

Ili kuzuia jambo hilo, usiku wa watu hukesha usiku kucha wakiwalinda ili wasitoke mwilini. Desturi hiyo ndiyo iitwayo .

iliingia kutoka China katika karne ya 8 (enzi ya Nara) na ilishamiri miongoni mwa wakuu hadi karne ya 12 (enzi ya Heian). Kati ya karne ya 17 na ya 19 (enzi ya Edo) iliungana na Ubuddha na Ushinto, ikaenea na kupendwa na watu wa kawaida. Hata leo, makumbusho kama vilima vya (庚申塚) na nguzo za (庚申塔) yamesalia kote nchini Japani, yakishuhudia ustawi wa desturi hiyo wakati ule.

Wadudu watatu waitwao sanshi: Joshi, Chushi na Geshi.
Wadudu watatu () — (juu), (kati) na (chini). Kutoka kitabu cha Kitao Taijo-jo-sanshi-chu-hosei-kyo.

Pakua PDF

Tokyo Koshindo ni kikundi cha watu wanaotekeleza na kujitahidi kuihuisha tena.

Tokyo Koshindo
Anwani: Mukoujima 3-7-4 Sumida-ku, Tokyo
www.koshindo.com